Psalms 74

Maombi Kwa Ajili Ya Taifa Kuokolewa

(Utenzi Wa Asafu)


1 aEe Mungu, mbona umetukataa milele?
Mbona hasira yako inatoka moshi
juu ya kondoo wa malisho yako?

2 bKumbuka watu uliowanunua zamani,
kabila la urithi wako, ambao uliwakomboa:
Mlima Sayuni, ambamo uliishi.

3 cGeuza hatua zako kuelekea magofu haya ya kudumu,
uharibifu wote huu ambao adui ameuleta pale patakatifu.


4 dAdui zako wamenguruma pale ulipokutana nasi,
wanaweka bendera zao kama alama.

5 eWalifanya kama watu wanaotumia mashoka
kukata kichaka cha miti.

6 fWalivunjavunja milango yote iliyonakshiwa
kwa mashoka na vishoka vyao.

7 gWaliteketeza kabisa mahali pako patakatifu,
wakayanajisi makao ya Jina lako.

8 hWalisema mioyoni mwao,
“Tutawaponda kabisa!”
Walichoma kila mahali ambapo Mungu
aliabudiwa katika nchi.

9 iHatukupewa ishara za miujiza;
hakuna manabii waliobaki,
hakuna yeyote kati yetu ajuaye
hali hii itachukua muda gani.


10 jEe Mungu, mtesi atakudhihaki mpaka lini?
Je, adui watalitukana jina lako milele?

11 kKwa nini unazuia mkono wako,
mkono wako wa kuume?
Uutoe kutoka makunjo ya vazi lako
na uwaangamize!


12 lLakini wewe, Ee Mungu, ni mfalme wangu tangu zamani,
unaleta wokovu duniani.

13 mNi wewe uliyeigawanya bahari kwa uweza wako;
ulivunja vichwa vya wanyama wakubwa wa kutisha katika maji.

14 nNi wewe uliyeponda vichwa vya Lewiathani
Lewiathani ni mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa.

nawe ukamtoa kama chakula
kwa viumbe vya jangwani.

15 pNi wewe uliyefungua chemchemi na vijito,
ulikausha mito ambayo ilikuwa ikitiririka daima.

16 qMchana ni wako, nao usiku ni wako pia,
uliziweka jua na mwezi.

17 rNi wewe uliyeiweka mipaka yote ya dunia,
ulifanya kiangazi na masika.


18 sEe Bwana, kumbuka jinsi mtesi alivyokudhihaki,
jinsi watu wapumbavu walivyolitukana jina lako.

19 tUsiukabidhi uhai wa njiwa wako kwa wanyama wakali wa mwitu;
usisahau kabisa uhai wa watu wako wanaoteseka milele.

20 uLikumbuke agano lako,
maana mara kwa mara mambo ya jeuri
yamejaa katika sehemu za giza nchini.

21 vUsiruhusu walioonewa warudi nyuma kwa aibu;
maskini na wahitaji hebu walisifu jina lako.


22 wInuka, Ee Mungu, ujitetee;
kumbuka jinsi wapumbavu
wanavyokudhihaki mchana kutwa.

23 xUsipuuze makelele ya watesi wako,
ghasia za adui zako, zinazoinuka mfululizo.
Copyright information for SwhKC